ARSENAL NA TOTTENHAM HOTSPURS WAINGIA KWENYE VITA KWA KUTUPA KARATA ZAO MPAKA MADRID

Mahasimu wa London Arsenal na Tottenham Hotspur zimeripotiwa kupigana vikumbo kuiwaina saini ya Isco wa Real Madrid
Kwa mujibu wa chanzo cha Hispania Diario Madridista, mkataba wa Isco unafikia mwisho 2018 na Real Madrid wanashawishika kumuuza msimu ujao badala ya kumpa mkataba mpya.
Arsenal na Spurs ndizo klabu mbili anazoweza kujiunga nazo, kadhalika Manchester City ambayo pia imekuwa ikivutiwa naye kwa muda mrefu na kurejea Malaga unaweza kuwa moja ya karata anazoweza kuchagua.

Leave a Comment