AGIZO LA TCRA KWA WAFANYABIASHARA NA WATUMIAJI WA SAMSUNG GALAXY NOTE 7

POSTED BY Mohamed Kaburu.
MAMLAKA
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepiga marufuku uingizaji na usambazaji
wa simu za mkononi za Smartphone Samsung Galaxy note 7 kwa kuwa zina
matatizo ya betri.
TCRA pia imewataka wananchi ambao tayari wanatumia simu hizo kuzizima na kuzirudisha haraka katika maduka walikozinunua.
Meneja
Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy, amewataka watanzania wajihadhari
kuitumia simu hiyo kwa kuwa Kampuni ya Samsung yenyewe imeiondoa sokoni.
“Simu hiyo tayari Samsung wenyewe wamesema ina matatizo ya betri na mara mbili sasa imelipuka,” amesema Mungy.na hata simu zilizotoka mara ya pili kumekuwepo na tatizo lile lile.
Amewaomba watu wenye simu za aina hiyo kuzirudisha madukani haraka wabadilishiwe ama kurudishiwa fedha zao.
“Hata kama uliletewa zawadi kutoka nje ya nchi nawaomba warudishe huko kuepuka matatizo yanayoweza kujitokeza,” amesema Mungy.
Hivi karibuni simu aina hiyo iliyothibitishwa na kampuni hiyo kuwa ilikuwa salama, ilishika moto kwenye ndege nchini Marekani.
Simu hiyo inadaiwa kushika moto ikiwa mikononi mwa abiria aliyekuwa kwenye shirika la ndege la Southwest Airlines.
Shirika
hilo liliwaondoa kwa dharura abiria waliokuwa kwenye ndege iliyokuwa
imepangiwa kusafiri kutoka Louisville, Kentucky, hadi Baltimore,
Maryland muda mfupi kabla ya kupaa.pia kampuni hyo ilitegemea kuletwa kwa note 7 kutaleta ushindani kwa Apple ambao nao wametoa iphone 7 lakini haikuzaa matunda matokeo yake simu hzo kuripotiwa kwa matukio ya kulipuka na hali hii sio tu Tanzania nchi nyingi zimepiga marufuku note 7 na kwamba ata ukiwa una safiri unatakiwa utoe betri na wala bila kuiweka kwenye umeme wakati ndege ikiwa angani kuepusha kusababisha madhara.
Leave a Comment