YANGA KUISHTAKI STAND UNITED KWA KUMTUMIA MCHEZAJI UYU KIMAKOSA

Hafidh Salehe - Yanga

Yanga inadai Stand United imemtumia Frank Khamisi kimakosa kwa kuwa bado ni mchezaji halali wa Polisi ya Zanzibar
Klabu ya Yanga imeikatia rufaa klabu ya Stand United ya Shinyanga kwa kosa la kumchezesha mchezaji Frank Khamisi katika mchezo wa ligi ya Vodacom uliopigwa Uwanja wa Kambarage na mabingwa hao watetezi kufungwa bao 1-0.
Meneja wa klabu ya Yanga Hafidh Salehe amesema, tayari wamewasilisha rufaa yao Shirikisho la soka Tanzania TFF, kwa sababu wana uthibitisho wa kutosha kutoka kwenye klabu ya Polisi Zanzibar aliyokuwa akiichezea kabla ya kutua Stand United.
“Tupo Pemba kujiandaa na mchezo wetu wa Jumamosi dhidi ya Simba lakini tumeshawasilisha rufaa yetu kwa TFF, kupinga Khamisi kutumiwa na United  katika mchezo wa Jumamosi kwa sababu tunavyo vithibitisho vya kutosha hadi barua ya chama cha soka cha Zanzibar ZFA, ikiwataka Stand wasimtumie mchezaji huyo hadi watakapokamilisha taratibu zao,” amesema Salehe.
Yanga inadai Stand United imemtumia Igobela kimakosa kwa kuwa bado ni mchezaji halali wa Polisi ya Zanzibar.
Chanzo cha habari kutoka Yanga SC kimesema kwamba, klabu imepata taarifa za kutosha kutoka Polisi ya Zanzibar juu ya mchezaji huyo.
Mbali na uthibitisho huo Yanga inadai mchezaji huyo alicheza mchezo huo bila kuwa na leseni inayomruhusu kucheza mchezo huo ambao ulikuwa ni wa kwanza kupoteza baada ya kucheza mechi 35 na timu za ndani ya Tanzania bila kupoteza.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.