UCHUMI: JE WEWE NI MMILIKI WA HISA? SOMA TAARIFA HII KUTOKA DSE JUU YA KUSHUKA KWA MAUZO YA HISA
Habari kamili mtu wangu wa sirini ni kwamba mauzo katika soko la hisa Dar es Salaam (DSE) yameshuka kwa asilimia 81 kutoka sh 9 bilioni mpaka kufikia Sh 1.7 bilioni. Na hii imetokana na kushuka kwa idadi ya uuzaji wa hisa kufikia Sh 340,000 kwa wiki.
Akiongea na waandishi wa habari Meneja Miradi na Biashara wa Dar es
salaam Stock Exchange Bw. Patrick Mususa alisema kuwa hata hivyo idadi
ya mtaji katika soko umekuwa kutoka tilioni 21.9 hadi tilioni 22.3 ikiwa ni sambamba na idadi ya mtaji wa makampuni ya ndani imekua tilioni 9.9.
Aidha Bw. Mususa ameitaja benki ya CRDB kuwa ndiyo imeongoza kwa kuuza hisa zake katika soko ikiwa na asilimia 92 zikifuatiwa na Kampuni ya Swissport yenye asilimia 4 na Twiga Cement ambayo ina asilimia 1.
“Kampuni ambazo zimeongoza kwa ongezeko la bei katika soko la hisa ni Kenya Airways yenye asilimia 9 pamoja na Kampuni ya bia ya East Africa Breweries ambayo ina asilimia 6 pamoja na Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia yenye asilimia 3”,alisema Bw.Mususa.

Je unalizungumziaje hili mwanajamii mwenzangu katika kijiji cha siri? Niandikie hapo chini
Kwa siri kama hizi na siri nyingine nyingi katika nyanda zote za burudani, biashara, siasa, kilimo , michezo na mengine mengi, usisahau kusubscribe, kulike, comment na kushare katika page zetu za Facebook na Instagram zinazokwenda kwa jina la "SIRI ZA JAMII"

Leave a Comment