TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA



Niklas sule




Chelsea wameingia kwenye ushindani mkali na liverpool kwa kumtolea macho mchezaji ambe alikuwa akiwaniwa mda mrefu na club ya  Liverpool katika Lengo la kumwania Niklas Sule ikiwa ni taarifa zilizotolewa na wakala wa beki huyo wa Hoffenheim . Tetesi hizi zimevuka mipaka  ikiwa team kama Reds , pamoja na Wolfsburg, Borussia Dortmund, Bayer Leverkusen , AC Milan , Napoli na Roma, wamekuwa wanaohusishwa na kumwania mkali hyo wa Hoffeinheim.

Mwakilishi wa Niklas Sule , Karl-Heinz Forster , alizungumza kwa waandishi wa habari kwa kusema : "Ndiyo, matamanio yalikuwepo alikuwa huko na waingereza wameweka wazi kwamba maslahi yao mwaka ujao bado ni halali. ".

Mchezaji hyo mwenye umri wa miaka 21 wa kimataifa raia wa Ujerumani ameripotiwa kuwa na furaha kwa kulipwa zaidi katika kikosi cha kwanza na Hoffenheim kabla ya kufanya maamuzi katika kupiga hatua nyingine ambayo ni ya pili katika kazi yake.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.