YANGA: TAMBWE AMEBUNI NJIA MPYA YA UPACHIKAJI MAGOLI BAADA YA KUONA USHINDANI KUTOKA KWA MAVUGO




Tambwe aibuka na njia mpya ya kuendeleza makali


Tambwe amebuni njia mpya itakayomfanya aweze kuteteza tuzo yake ya ufungaji bora baada ya kuona ushindani mkubwa kutoka kwa Laudit Mavugo.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi anayeichezea klabu ya Yanga Amissi Tambwe, amesema amebuni njia mpya itakayomfanya aweze kuteteza tuzo yake ya ufungaji bora baada ya kuona ushindani mkubwa kutoka kwa Laudit Mavugo.
Mfungaji huyo bora wa msimu uliopita ameiambia Gola, amepanga kuitumia vema kila nafasi atakayoipata katika kila mchezo atakaopangwa kuanzia mechi ya Jumapili ambayo watacheza ugenini dhidi ya Stand United ya Shinyanga.

“Msimu huu ligi ni ngumu na ushindani wa kufunga mabao unaonekana ni mkubwa ndiyo maana nimeamua kuongeza umakini kwa kuzitumia vizuri nafasi ninazo zipata ili kutetea tuzo yangu lakini pia kuipa ubingwa watatu mfululizo timu yangu ya Yanga,”amesema Tambwe.
Tambwe na Mavugo kila mmoja amefunga mabao matatu tangu kuanza kwa msimu huu lakini Tambwe anapewa nafasi kubwa kutokana na uzoefu aliokuwa nao kwenye ligi ya Vodacom ambayo huu ni msimu wake wa nne na ameweza kutwaa tuzo hiyo mara mbili.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.