SIRI ZA JAMII: USAJILI WA KAMPUNI NA TARATIBU ZAKE FAHAMU HAPA
Posted by Jackson Msuya
USAJILI MWA KAMPUNI
Taratibu za Usajili wa Kampuni BRELA
Utaratibu Muda, siku, Gharama(ada)
Pata kibali toka BRELA kuhusu jina linalopendekezwa kuwa liko huru kwa kuwasilisha maombi ya jina. Maombi ya kusajili jina (Fomu Namba 8) yanaweza kuwasilishwa kwa barua kwa Msajili wa Makampuni au kwa kufika kwenye Ofisi za BRELA. Baada ya kupata uthibitisho kuwa jina linakubalika, Mwombaji anatakiwa kuandaa na kuwasilisha Hati za Kuanzisha Kampuni zikiwa na jina la kampuni lililokubaliwa. Mchakato wa kutafuta jina kama linafaa unaweza kufanywa pia kwa kutumia tovuti ya BRELA, yaani www.brela-tz.org
Siku 1 bila malipo.
Pata tamko la kiapo toka kwa mwanasheria kuwa una uhalali wa kufanya biashara Siku 1 Gharama za
kiapo kwa wanasheria ni kati ya Shilingi 10,000 na 50,000 kwa nyaraka za kawaida kama vile Fomu Namba 14b.
Omba na Pata Hati ya Kuandikishwa Majina ya Biashara (Sura ya 213) na Majina ya Kampuni (Sura ya 212). Hati ya kuandikishwa majina ya biashara na majina ya kampuni hufanyika Dar es Salaam pekee. Si lazima kutumia mwanasheria japo ni kawaida kufanya hivyo. Wakati wa kuomba hati ya kuandikishwa, sanjari na fomu ya maombi (Fomu Na. 1), Mwombaji, Mwanasheria au mtu aliyetajwa kwenye Hati za Kampuni kama Mkurugenzi, sharti awasilishe nyaraka zifuatazo kwa Msajili wa Makampuni,):
.. Fomu Na 14a (Wakurugenzi wa Kwanza, Katibu na Anwani ambapo ofisi zitakuwa)
.. Fomu Na 14b (Tamko la Kukiri Kufuata Taratibu za Kuandikishwa Kampuni.
.. Hati za Kuandikishwa Kampuni
Siku 4 Maombi ya kusajili jina hutozwa Sh 5,000 na utafutaji wa jina hutozwa Sh. 1,000. Ada ya mwaka ya kutunza jina la biashara au kampuni ni Sh. 1,000.
KUMBUKA: Pamoja na kutamkwa hivyo kisheria, kwa kawaida muda unaotumika kusajili jina la biashara ni siku 2.
Baada ya kujaza fomu, kwa kawaida Hati ya Kuandikishwa huandaliwa ndani ya siku 2-3. Fomu za usajili ni bure, isipokuwa ada za usajili hutegemea kiasi cha hisa za mtaji kama ilivyoonyeshwa hapo chini. Ada ya usajili wa kampuni yenye mtaji wa chini ya Shilingi Milioni Moja ni asilimia 10 ya mtaji husika.
VIWANGO VYA ADA KULINGANA NA HISA ZA MATAJI:
.. Hisa za mtaji kuanzia 20,000-500,000: Shilingi 50,000
.. Hisa za mtaji kuanzia 500,000-1,000,000: Shilingi 80,000
.. Hisa za mtaji kuanzia 1,000,000 – 2,000,000: Sh. 100,000
.. Hisa za mtaji kuanzia 2,000,000 – 3,000,000: Sh. 120,000
.. Hisa za mtaji kuanzia 3,000,000 – 5,000,000: Sh. 150,000
.. Hisa za mtaji kuanzia 5,000,000 – 10,000,000: Sh. 180,000
.. Hisa za mtaji kuanzia 10,000,000-30,000,000: Sh. 200,000
.. Hisa za mtaji kuanzia 30,000,000 na zaidi: Sh. 300,000 Ada ya jalada: Sh. 45,000 (15,000 kwa kila nyaraka) Ada ya ushuru wa stempu:
.. Nakala halisi ya Hati za Kampuni: Sh 6,200
.. Nakala za ziada: Sh. 5,000
Gharama za usajili wa makampuni zinategemea kiwango cha hisa za mtaji.
Omba Nambari ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Nambari ya Utambulisho wa Mlipa Kodi hutolewa bure. Mchakato mzima unafanyika kwa njia ya kompyuta na nambari yaweza kupatikana ndani ya siku 1 au 2 kutegemea idadi ya maombi katika ofisi za TRA. Wakati wa kuomba nambari ya utambulisho wa mlipakodi mwombaji sharti aambatishe nakala ya Hati ya Kuandikishwa Kampuni kutoka BRELA na Hati ya
Kampuni. Wakati wa kuomba Hati ya Utambulisho wa Mlipa Kodi, kampuni itapaswa kuwasilisha:
.. Maombi ya hati kwa ajili ya Kampuni
.. Maombi ya hati kwa kila Mkurugenzi/mwanahisa wa Kampuni endapo Mkurugenzi huyo hatakuwa na nambari yake ya utambulisho tayari.
Siku 1 Hakuna malipo
Pata Nambari ya Utambulisho wa Mlipa Kodi. Wakurugenzi wote wa Kampuni sharti wafike kwenye ofisi za TRA kwa ajili ya kuchukuliwa alama za vidole. Mwombaji sharti afike mwenyewe kwenye ofisi za TRA kuchukua Hati ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN). Kampuni itatakiwa kukisia mapato yake katika mwaka huo kwa ajili ya makadirio ya kodi kwa upande wa TRA. TRA pia yaweza kuwahoji wakurugenzi na kuchukua kumbukumbu kuhusu biashara na maelezo yao binafsi.
Siku 1 Hakuna malipo.
Omba Leseni ya Biashara kutoka kwa Mamlaka Husika (Afisa Biashara wa Halmashauri au Wizara kutegemea aina ya biashara). Leseni ya biashara yaweza pia kutolewa na masharti au tozo fulani moja kwa moja.
Fomu ya maombi ya leseni hulipiwa Shilingi 1,000. Wakati wa kuwasilisha maombi, mwombaji atatakiwa aambatishe nakala za nyaraka au uthibitisho ufuatao:
1. Hati ya Kuandikishwa Kampuni
2. Hati ya Kuanzisha Kampuni
3. Uthibitisho wa Uraia wa Tanzania
4. Uthibitisho wa kumiliki sehemu ya biashara
5. Nambari ya Utambulisho wa Mlipa Kodi
Siku 6 Shilingi 1,000.
Omba Hati ya Kusajiliwa kama Mlipaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT). Hati hii hutolewa kwa kampuni yenye mapato yanayotozwa kodi yanayozidi Shilingi Milioni 40 kwa kipindi cha kuanzia miezi 12 inayofuatana au mapato yatakayozidi Shilingi Milioni 10 katika kipindi cha miezi mitatu itakayofuatana. Usajili huchukua siku 3-5
Siku 4 Hakuna malipo.
Andikisha kampuni kwa ajili ya Bima ya Wafanyakazi kwa Shirika la Bima la Taifa au kampuni nyingine yoyote ya bima. Maombi ya bima ya wafanyakazi sharti yafanywe kabla kampuni haijaanza kazi. Siku 1 Hakuna malipo.
Andikisha kampuni katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kama vile NSSF, PPF au mfuko mwingine. Kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Jamii, kila mwajiri lazima asajili wafanyakazi wake katika mojawapo ya mifuko ya hifadhi ya jamii. Hata hivyo, mfanyakazi anaweza kuamua mwenyewe ajiunge na mfuko upi.
Siku 7 Hakuna malipo

Leave a Comment