SINGIDA: KIJANA ANYOFOLEWA ULIMI AKINYONYANA NDIMI

Tukio hili la mwanaume huyu kung'atwa na hatimae kung'olewa kipande cha ulimi limetokea huko Singida.
Ni kweli mtu unaweza kuwa na hisia za kimapenzi na mtu mwingine ulioonana nae mahala lakini kitendo cha kuchukua maamuzi ya kukiss au kufanya mapenzi inaitaji mtu muwe mmejuana kidogo na tuwe makini tunapokutana na watu na kuwaamini kupita kiasi natoa pole na liwe ni fundisho pia katika jamii.
Mkazi wa Mandewa, Manispaa ya Singida, Said Mamba (24), amelazwa katika hospitali ya mkoa mjini Singida baada ya kung’atwa theluthi tatu ya ulimi wake na mwanamke waliyekuwa wakinyonyana ndimi.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Septemba 12, saa 3:30 usiku wa sikukuu ya Idd el Hajj.
Mamba, ambaye hawezi kuzungumza ametoa maelezo ya tukio hilo kwa njia ya maandishi.
Alisema siku ya tukio alikutana na mwanamke huyo kwenye grosari iliyopo eneo la Mandewa na baadaye mwanamama huyo alimwomba amsindikize nyumbani kwake.
“Nilikubali kumsindikiza, tukiwa njiani aliniomba tufanye mapenzi. Nilipokataa alinilazimisha na baada ya kuona sitaki aliomba tuagane kwa kunyonyana ndimi, nilikubali ombi hilo,” alisema.
Mamba alisema wakati wakiendelea, mwanamke huyo alianza kumvua mkanda wa suruali lakini alimzuia ndipo alipomng’ata ulimi na kuondoka na kipande.

Leave a Comment