SHERIA: UNATAKA KUPATA MKOPO KWA KUWEKA ARDHI YAKO REHANI? FAHAMU TARATIBU ZAKE


Taratibu za Kufuata ili Kupata Mkopo kwa Kuweka Ardhi Rehani Ili muweka rehani aweze kupata mkopo kupitia taasisi za fedha ni muhimu afanye mambo yafuatayo:

i. Ahakikishe kwamba ana hati miliki ambayo imelipiwa ada zote zinazohitajika kisheria
 

ii. Mwombaji awe na taarifa/ripoti ya tathmini ya ardhi

iii. Atembelee taasisi za fedha kwa ajili ya mazungumzo ya awali na kufanya tathmini ya thamani ya ardhi husika


iv. Kama mazungumzo ya awali yatakuwa yamekubalika mwombaji wa mkopo atalazimika kufanya maombi ya awali kimaandishi. Maombi hayo yataainisha madhumuni au sababu za mkopo na namna ya kuurejesha, n.k


v. Endapo maombi yake yatakubalika, mwombaji atalazimika kujaza fomu maalumu ambayo itaonesha jina halisi la mkopaji, majina ya mwenza (mke au mume), anuani halisi ya makazi, kiwango cha mkopo, namna ya kurejesha mkono, kutia saini fomu ya mkopo na endapo ardhi inayotumika ni mali ya familia basi mwanandoa ni lazima atie saini pia


vi. Kutoa taarifa sahihi na kuambatanisha nyaraka zote kama vile taarifa ya tathmini kukamilisha maombi ya mkopo.


Endapo taasisi ya kifedha itajiridhisha na maombi ya mwombaji basi itakuwa tayari kutoa mkopo kwa mwombaji na atapata mkopo wake kupitia akaunti ya benki itakayokuwa imefunguliwa katika benki hiyo.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.