SHERIA: SIRI ILIYOPO KATIKA UKAMATWAJI WA MTUHUMIWA KATIKA MFUMO WA JINAI



Zijue Haki za Raia katika Mfumo Jinai
|
Kukamatwa kwa Mtuhumiwa
Taratibu za nchi kupitia sheria mbalimbali zimeweka bayana mtu
au chombo chenye mamlaka ya kumtia mtu nguvuni. Kwa mujibu
wa taratibu za nchi ya Tanzania, wafuatao ndio wenye mamlaka ya
 kumtia mtu nguvuni:


  1. Askari polisi,
  2. Mgambo na Sungusungu
  3. Mtu binafsi,
Hakimu wa Mahakama yeyote.
Kwa kawaida, mtuhumiwa anakuwa ametiwa nguvuni pale
atakapozuiliwa na polisi na kuondolewa haki yake ya kwenda
atakako. Lengo kuu la kufanya hivyo ni kumweleza mtuhumiwa kosa
analotuhumiwa nalo na pia kutoa mwanya kwa mamlaka yaani polisi
au chombo kingine kama vile TAKUKURU kufanya upelelezi wa
kutendeka kwa kosa la jinai. 
Mtuhumiwa anapokuwa ameshukiwa kuhusika katika kutenda kosa,
na wakati askari polisi anapokuwa akifanya kazi ya upelelezi wa kosa
la jinai anayo mamlaka ya kumzuia mtuhumiwa kwenda atakako
hata kama polisi anayehusika na zoezi hilo hana uhakika kama mtu
anayemzuilia ametenda kosa husika au anahusika katika kosa hilo.
Mtu atahesabika kuwa ametiwa nguvuni ikiwa atazuiliwa kuondoka
na kwenda atakako kutokana na kuwa nguvuni; au kutendeka kwa
kosa la jinai na polisi anaamini kwamba mtu huyo ametenda kosa
hilo la jinai. Katika mazingira haya, sheria inampa polisi mamlaka ya
kumkamata mtu huyo bila ya kuwa na hati ya kumkamata.
Mazingira yafuatayo yanampatia mtu binafsi au askari polisi haki ya
kumkamata mtuhumiwa bila ya kuwa na hati ya kukamata (Warrant
of Arrest) 
a
 mtu atakayefanya tendo la kuvunja amani mbele ya askari,
b. mtu anayemzuia askari polisi kufanya kazi zake, au atafanya
jaribio la kutoroka au atatoroka kutoka chini ya ulinzi.
c.
mtu atakayeonekana kuwa na mali ya wizi au inayoshukiwa
kuwa ya wizi,
d.
mzururaji au mtu anayezurura kwa nia ya kufanya uhalifu,
e.
mtu anayeshukiwa kuwa hati ya kukamatwa imeshatolewa
dhidi yake,
f.
mtu yeyote ambaye amefanya kosa nje ya Tanzania na kuna
uwezekano wa kuadhibiwa ndani ya Tanzania,
g.
mtu anayedharau nembo ya taifa kama vile wimbo wa Taifa
au Bendera ya Taifa
Endapo mtuhumiwa atakamatwa na raia, basi ni wajibu wa
raia kumfi
kisha mtuhumiwa mbele ya kituo cha polisi haraka
iwezekanavyo

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.