SERGE WAWA SASA YUKO FITI KUIKABILI RUVU SHOOTING

Azam FC itahitaji ushindi dhidi ya Ruvu Shooting
katika mechi yao ya Jumamosi na kocha mpya Azam kwa mara ya kwanza
atamtumia Serge Wawa
Daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa amesema, kuwa Wawa ameanza mazoezi mepesi wiki mbili zilizopita na kwa sasa yupo fiti kwa ajili ya mikiki-mikiki ya ligi ya Vodacom Tanzania.
“Unajua tayari tumepoteza michezo miwili niwazi timu inaonekana kuwa na mapungufu hasa kwenye sehemu ya ulinzi sasa kupona kwa Wawa kunaweza kukawa msaada kwa kocha Hernandez ambaye kiukweli anaumiza kichwa kuona kikosi chake kinafanya vizuri,” amesema Mwankemwa.
Azam itapambana na Ruvu Shooting, kwenye uwanja wake wa nyumbani na itahitaji ushindi baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Simba na Ndanda FC
s

Leave a Comment