PICHA :AJALI ILTOKEA KATIKATI YA MSAFARA WA MAKAMU WA RAISI MH SAMIA SULUHU AKIELEKEA MTWARA
Ni leo ijumaa ambapo Msafara wa makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassani ambao ulikuwa unaelekea wilayani tandahimba ukitokea ikulu ndogo ya rais mtwara umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa ligula.
Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji
cha nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya mtwara,majeruhi
walioumia ni dereva pamoja na wasaidizi wanne wa makamu rais.
Gari hilo lililobeba
wasaidizi wa rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba
waandishi wa habari liliacha njia na nusura kupinduka.
Barabara ya kutoka mtwara kuelekea
tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda
mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka
kabisa na kusababisha majeruhi.

Leave a Comment