NGASA AFUZU MAJARIBIO KUKIPIGA KWENYE CLUB YA OMAN



Fowadi wa Free State ya Afrika Kusini Mrisho Ngassa katika mazoezi Stars


Baada ya kuachana na Free State Ngasa alitaka kurejea Yanga lakini kocha Hans van der Pluijm, akamgomea na kuamua kutimkia Oman ambapo amefanikiwa sasa
Mshambuliaji wa zamani wa Free State na Yanga Mrisho Ngassa hatimaye amefuzu majaribio kwenye klabu ya Fanja huko Omon na tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo.
Ngassa aliyevunja mkataba wa kuitumikia Free State ya Afrika Kusini wiki tatu zilizopita ameiambia Goal, kwa njia ya mtandoa wa Fecebook, kwamba majaribio yake yalikwenda vizuri na amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo.
“Nashukuru majaribio yangu yalikwenda vizuri na kocha amekubali uwezo wangu na moja kwa moja amenipa mkataba wa miaka miwili hivyo kwasasa mimi ni mchezaji halali wa Fanja,”amesema Ngassa.
Baada ya kuachana na Free State Ngasa alitaka kurejea Yanga lakini kocha Hans van der Pluijm, akamgomea na kuamua kuitwa Oman kwa majaribio kwenye klabu ya Fanja na hatimaye amefanikiwa na sasa atajiunga na timu hiyo mara moja baada ya kukamilisha taratibu za kufanya kazi falme za kiarabu.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.