NENO KWA VIONGOZI WA BAADAE, BABA NA WALEZI


2 september 2016
posted by Uncle Nyoni
Unapozaliwa mtoto wa kiume unakuwa ni kichwa cha familia kwa hyo ata unapondenda mambo yako ilo likae kichwani kwamba wewe ni kichwa na ni kiongozi kwa ujumla kwa sababu ni mzigo mzito kama walivyo imba wana Msondongoma kwamba "kuzaliwa mwanaume ndio ujue kila kitu kwako kitakuwa ni tabu kwa hyo kupambana na maisha ni jambo la msingi sana" mwanaume ambae ni smart alafu akizungukwa na wanaume wengine katika kushirikiana kutoa maamuzi hayo maamuzi hua ni mazuri na makubwa.

Lakini wengi wetu tunakosa mambo haya, watu wa mjini huita bongo lala kwa kutoka kujua sisi ni akina nani na wapi tunasimamia kwa kuamini tumelala na bundi yani tuna bahati mbaya kwa kudhani tuliumbwa kwa nyiongeza kwa kuamini kwamba wengine waliofanikiwa ni wateule kwa sisi kama tuna dhiki basi tufe nazo kitu ambacho ni fikra potofu
 Wewe kama mwanaume upewi kitu inakubidi kutafuta kufanya kazi kwa bidii mjini hapa kwanza upole ulionao utakushinda kama ulivomshinda yesu akavunja sinagogi itakua wewe? kuna vitu vya kujitofautisha na watu wengine ukikomaa na kutoa kila unachokipata wenzako watafurahia maisha wakati wakiwa na vitu ulivyowasaidia na wewe ukabaki hauna kitu ndio maana tunasema unapokuwa na familia hao ndio ndugu zako na uwe na macho ya kuona nani rafiki wa kweli sababu tunaimbiwa kwenye nyimbo kila siku rafiki wa kweli kama ndoa upo nae kwenye shida na kwenye raha sio yule ambae upo nae kwenye ofa za bia alafu kwenye matatizo anageuka hussein bolt hao sio watu jiweke nao ambali awawezi tu kukurudisha nyuma bali na kuyadidimiza maisha yako.
Saw sikatai mwanaume inabidi ulinde familia lakini angalia familia gani unailinda je ni ya yule msichana aliekukataa na kukutukana? au ya yule rafiki ambae anakusnitch kila ukimpa kisogo au unalea sana washkaji na kusahau majukumu mengine ya maisha na watu muhimu katika maisha yako. Fanya maamuzi ya kiume sasa kwa kuwa na msimamo kwa killa kitu unachamua ukiendelea kutoa macho kama chura aliekosa maji shauri ako wenzio watakupiku wewe utabaki palepale.
Kumbuka kwamba unailisha familia yako kwanza kabla ya kulisha familia ya mlango wa pili kwa sababu damu mnayoshare ni kitu muhimu sana katika hii dunia kwa hyo unakuwa unalisha damu yako mwenyewe unafanya jambo hili kwanza kwa nguvu zote alafu unafikiria mlango wa pili lakini ni mwiko kutoa sehemu nyingine kiwango kile kile kama unachotoa kwenye familia yako na utajiri utakao pata ni wa kwako na damu yako.
Sio kila kiumbe katika dunia hii kina staili ulichonacho wewe waache wapate kile wanachostaili kama ni kuzimu wamejitengenezea basi shauri yaho ndo maana waswahili wanasema fongo alikosa mkia kwa sababu ya kulala wanasema na ukilala utakila unachokiota sasa mwenzetu ukiota mti wewe kula mzizi kiroho safi maisha yamekushinda tafuta sehemu ambapo ni marahisi hapa mjini utakuja kuwatafutia watu lawama bure kwa uchovu wako. Japo kusaidiana kupo katika matatizo mbali mbali lakini pia sio mbaya mtu ukibebwa jishike na wewe unapewa mtaji heshimu pesa za watu na uzifanyie mambo ya msingi uwezi jua watu wametafutaje icho kidogo walichokusaidia wewe ujikwamue, mimi nimemaliza jamani niwatakie mapumziko mema.

 

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.