Luke Shaw hatacheza dhidi ya Northampton Kombe la EFL, lakini nyuma ya pazia nyota huyo ameeleza jinsi alivyokerwa na kocha wake Jose Mourinho
Beki wa kushoto wa Manchester United Luke Shaw imeripotiwa kuwa haifurahii tabia ya Jose Mourinho kumkosoa mbele ya umma kufuatia kipigo cha Watford cha Jumapili.
Meneja huyo wa United alidai kuwa Shaw alifanya kosa la 'kimbinu na kiakili' kwa kutomkaribia vema Camilo Zuniga ambaye alifunga goli timu yao ikiangukia pua kwa kichapo cha 3-1 katika Vicarage Road.

Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza, aliyekuwa kwenye matibabu miezi nane msimu uliopita,  anasumbuliwa na majeraha.

Nyuma ya pazia, Shaw ambaye alitolewa mchezoni dakika za mwishoni kipindi cha pili dhidi ya Watford, hajafurahishwa na namna Jose Mourinho alivyomkosoa hadharani baada ya mechi.
United wamepoteza mechi tatu mfululizo katika michuano yote.