HIKI NDICHO KITAKACHO KUKUTA UKISHINDWA KULIPO MKOPO ULIOKOPA BENKI


Matokeo ya Kushindwa Kulipa Mkopo.

a. Mkopaji hupewa taarifa ya siku 60 kwa maandishi kuwa
nyumba/ardhi yake itauzwa kwa njia ya mnada;
b. Mkopeshaji huuza nyumba au ardhi kwa njia ya mnada;
c. Nyumba hupigwa mnada kwa kutoa taarifa (notisi) ya siku 10 kwa mkopaji na wanaoishi kwenye nyumba.


Angalizo: Kwa mujibu wa Sheria, mtu yeyote atakayetoa maelezo kuwa aliweka rehani ardhi yake kwa kushinikizwa, kigezo hicho si njia ya kumzuia mkopeshaji kuuza ardhi iliyowekwa rehani. Kadhalika, rehani ya kimila itafuata taratibu za kimila zinazotumika katika eneo hilo. Hata hivyo lazima zizingatie misingi ya haki kwa wahusika.



Taratibu za Kukomboa Fedha Endapo Mweka Rehani Atashindwa Kulipa Mkopo Kwa mujibu wa Sheria za Ardhi, taasisi ya fedha inaweza kukomboa fedha zake kwa mkopaji kwa:
a) Kutoa taarifa kwa umma ya kuuza ardhi ili kukomboa fedha zilizokopeshwa kwa mkopaji;
b) Taarifa ya mauzo itokayotolewa kwa umma itolewe pia kwa mtu yeyote mwenye maslahi kwenye ardhi husika kwa muda usiopungua siku kumi;
c) Kuuza ardhi ya mkopaji kwa njia ya mnada wa hadhara; Kiujumla, taasisi ya fedha au mkopeshaji yeyote haruhusiwi kujiuzia ardhi au nyumba iliyowekwa dhamana. Hata hivyo, taasisi inaweza kujiuzia ardhi iliyowekwa dhamana kama atakuwa amepata ruhusa ya mahakama na atanunua kupitia mnada wa hadhara na awe na dau la juu kuliko wote.


KUMBUKA: Tofauti na sheria ya zamani ambapo mkopeshaji hakutakiwa auze nyumba iliyowekwa rehani bila kibali cha mahakama iwapo nyumba hiyo ni nyumba ya kuishi au ardhi kwa ajili ya kilimo, Sheria ya sasa kama ilivyorekebishwa na sheria ya mikopo ya ujenzi wa nyumba ya mwaka 2008 inampa uwezo mkopeshaji kuuza nyumba au ardhi ya mkopaji baada ya kuisha muda wa notisi hata kama nyumba inayouzwa ni ya kuishi au ni ardhi ya kilimo.

Mahakama Kuu inayo nguvu ya kusitisha uuzaji wa nyumba iliyowekwa rehani endapo mkopaji ataenda kuomba kusitishwa kwa uuzaji huo. Hii itawezekana kama Mahakama Kuu itaona kuwa kuna uwezekano wa hali ya juu sana kwamba mkopaji ataweza kulilipa deni iwapo atapatiwa muda kidogo au nyumba iliyowekwa rehani ni ya thamani ya kutosha kiasi kwamba hataikichelewa kuuzwa deni litaweza kufidiwa na faini ya kuchelewa pia italipwa pindi ambapo kitauzwa.



No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.