HATUA CHACHE ZA MWANZO KATIKA KUSAJILI BIASHARA YAKO

AINA ZA USAJILI WA BIASHARA
Kuna hatua kadhaa za kufuata ili kusajili biashara yoyote nchini Tanzania. Kampuni inaweza kusajili jina la biashara kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Maombi ya Usajili wa Jina la Biashara hufanywa kwa kujaza Fomu Namba 8, na kuiwasilisha moja kwa moja BRELA. Kabla ya kuwasilisha jina linalopendekezwa mwombaji aweza kupitia tovuti ya BRELA, www.brela-tz.org, ili kujua kama jina hilo halimilikiwi na kampuni au biashara nyingine.

USAJILI WA BIASHARA
Kuna aina mbili za fomu za maombi ya usajili wa jina la biashara, moja kwa usajili wa mtu binafsi, na nyingine kwa usajili wa ubia. Taratibu za usajili ni pamoja na:
  1. Pata uthibitisho kutoka BRELA kuwa jina linalopendekezwa halimilikiwi na biashara nyingine
  2. Wasilisha fomu za maombi ya jina la biashara baada ya kulipia ada ya usajili katika Benki ya CRDB, Tawi la Lumumba, au benki nyingine iliyopendekezwa na BRELA .
  3. Hati ya kuthibitisha jina la biashara yaweza kuwa tayari kuchukuliwa baada ya juma moja au mawili tangu kuwasilishwa maombi ya usajili.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.