GARETH AJIPONGEZA KUINGOZA ENGLAND

Kaimu meneja wa timu ya taifa ya
England, Gareth Southgate amesema 'ilikuwa hatua muhimu' kuchukua nafasi
ya meneja wa zamani Sam Allardyce.
Southgate, ambaye wakati wa
uchezaji wake alikuwa beki, awali amekuwa akinoa timu ya vijana
chipukizi wenye chini ya umri wa miaka 21 na ataongoza klabu hiyo ya
taifa ya Uingereza kwa michuano minne ijayo.Allardyce aling'atuka siku ya Jumanne baada ya uchunguzi wa gazeti la Daily Telegraph kudai kuwa Allardyce, alitumia cheo chake kushiriki mpango wa pauni 400,000 na kutoa ushauri kuhusu vile watu wangeweza ''kukwepa'' sheria za uhamiaji wakati wa kuhama kwa wachezaji
Southgate, 46, amesema mwezi Juni hakuwa na matamanio yoyote ya kumrithi Roy Hodgson kama meneja wa timu hiyo.

Hata hivyo meneja wa Arsenal Arsene Wenger na Eddie Hodgson wa Bournemouth ambao wamehusishwa na matamanio ya kazi hiyo wameelezea jitihada zao kwa klabu zao.
Meneja wa Uingereza amesema nafasi hiyo ni kama 'wadhifa mkubwa', huku wenger amesema 'anaangazia' klabu ya Arsenal kwa asilimia 100.

Leave a Comment