EUROPA LEAGUE: MANCHESTER DIMBANI NA ZORYA LUHANSK



Manchester United


Kukutana na klabu ya Manchester United katika uwanja wa Old Trafford katika ligi ndogo ya klabu bingwa Ulaya, Europa League, siku ya Alhamisi itakuwa ya 'kuogofya' amesema meneja Yuriy Vernydub wa klabu ya Zorya Luhansk ya Ukraine.
Mechi hiyo itaanza saa nne na dakika tano usiku Afrika Mashariki.
Klabu hiyo ya Zorya Luhansk, ilimaliza katika nafasi ya nne katika ligi ya Ukraine msimu uliopita na wanaanza mechi yao ya kwanza katika hatua ya makundi.
''Hakuna sababu ya kujiepusha. Tunaelewa kwamba Manchester United ni klabu ya kimataifa,'' amesema Vernydub.
Nahodha wa United Wayne Rooney alikuwa anatarajiwa kujiunga katika kikosi cha kwanza cha watu kumi na moja lakini amekuwa na shida ya mgongo.

Wayne Rooney

Mshambuliaji huyo,30, aliachwa nje katika mechi iliyochezwa wikendi iliyopita katika ligi ya premia waliyoondoka na ushindi dhidi ya Leicester City.
Meneja Jose Mourinho amesema: ''Nilikuwa nimeamini kumchezesha kutoka mwanzo (siku ya Alhamisi) lakini kwa jinsi mambo yalivyo hivi karibuni sina uhakika.''
Mourinho amethibitisha mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, ataanza katika wachezaji 11 wa kwanza, lakini mashetani hao wekundu watamkosa kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan, huku Luke Shaw akiwa hajulikani hali yake baada ya kurudishwa nyumbani siku ya Jumatano kutokana na maradhi.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.