AJALI MAJI MATITU DALADALA KUGONGANA NA GARI TATU KWA MPIGO WANANCHI WATOA TAMKO
Posted by erastowambura@gmail.com on Tuesday, August 30, 2016
Mwanamke makzi wa chamanzi amejeruhiwa baada ya gari lake dogo
alilokuwa akiendesha kugongwa na daladala lenye namba T 397 BVB
linadodaiwa kuiba njia.
Daladala lenye namba za usajili T
397 BVB linalofanya safari zake kati ya Temeke na Gongo la Mboto kwa
kuyagonga magari matatu eneo la Maji Matitu Temeke Dar es Salaam
leo asubuhi. Katika ajali hiyo dereva wa gari dogo namba T 628 DFE
alijeruhiwa.
Daladala lililogonga gari namba T 458 CAN.
Kuku waliokuwa kwenye moja ya gari lililogongwa wanachi wakitoa msaada
Askari wa Usalama barabarani akiwa kazini mara baada ya ajali hyo.
Daladala llilpokutana uso kwa uso na vitz.
Mkazi
wa eneo hilo Hamisi Juma ameongea kwamba ni Mungu ndio amenusuru katika ajali hiyo maana ilikuwa ni mbaya sana
"
Saa 12 na dakika 55 nikiwa nasubiri gari kwenda kazini niliona daladala
lililokuwa likitoka Charambe kwenda Chamazi lilikuwa likipita upande
ambao si wake likiwa katika mwendo wa kasi na ghafla lililigonga gari
dogo ambalo likageuka na kulala katika mtaro" alisema
bwana khamis Juma.
Alisema
baada ya kuligonga gari hilo liliyaparamia magari mengine madogo mawili
likiwepo lililobeba kuku na kuyasukumia kwenye mtaro.
Aliongeza kuwa baada ya kutokea tukio hilo dereva wa daladala hilo alikimbia na kulitelekeza gari lake.
Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni T 628 DFE, T 397 BVB, T 451 CQB na T 458 CAN.
Jitihada
za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke ili kuzungumzia suala hilo
hazikuzaa matunda baada ya simu yake kuita bila kupokewa alipopigiwa
simu mara kadhaa.

Leave a Comment