ZIDANE HATAJISIKIA VIZURI AKIYASIKIA HAYA KUTOKA KWA RONALDO
Ronaldo ameshindwa kuficha jibu lake kutokana na swali gumu
aliloulizwa kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kusign
mkataba mpya na Nike. Kwenye moja ya maswali lilikuwa ni kocha yupo bora
kwake kwa sasa hivi.
Jibu halikua gumu kutoka kwa Ronaldo,“Ni wazi kwamba makocha
wangu wote wawili wamefanya kazi kubwa sana na timu zangu zote mbili
Real Madrid na Portugal. Sasa kwa mawazo yangu ni ngumu sana kushinda
ubingwa wa Ulaya na Portugal, ilikua ni mara yetu ya kwanza kwenye
historia. “
Ronaldo aliendelea,“Zidane amefanya kazi nzuri sana lakini
kwa sasa nampa favor Santos kama kocha bora. Hii haitokani kutokana na
uhusiano wangu na hawa wawili. Wote nipo nao vizuri kabisa na wanafanya
vitu vizuri kwangu. Lakini kwa sasa nampa Fernando Santos”
Leave a Comment