YANGA WALIVYOWATAWALA WAJELAJELA UWANJA WA SOKOINE JIJINI MBEYA
Hapo jana katika viwanja mbali mbali Tanzania bara, timu mbalimbali zilikuwa zinatimua vumbi ili kutetea point muhimu zitakazowapa nafasi nzuri katika msimamo wa ligi. Moja ya mchezo uliovuta hisia za watu wengi ni mechi kati ya Dar Young Africans "Yanga" na Tanzania Prisons. Mchezo huo uliisha kwa Yanga kushinda kwa bao moja lililofungwa na Simon Msuva kwa njia ya mkwaju wa Penalty katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Prisons walipata penalty baada ya Deus Kaseke kufanya madhambi katika eneo la hatari lakini mpiga penalty wa prisons Lambert Sabianka alipoteza penalty hiyo iliyookolewa na kipa Beno kakolanya.
Yanga pia walipata penalty baada ya mzambia obrey chirwa kufanyiwa madhambi, penalty hiyo haikufanyiwa makosa na mchezaji Simon Msuva.
Na hapa nimekuwekea picha zaidi za mtanange wa jana baina ya Yanga na Tanzania Prisons.
Leave a Comment