YANGA INA KIBARUA KIZITO MBEYA KWA WAJELAJELA, RATIBA NZIMA YA LIGI KUU BARA WEEKEND HII ITAZAME HAPA
Kesho Jumapili, African Lyon inatarajiwa kucheza na Simba kwenye
Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Mbao FC itakuwa mwenyeji wa Azam
FC Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kwa upande wake, Ndanda itakuwa mwenyeji wa Stand United ya Shinyanga
kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati Tanzania Prisons
inatarajiwa kuialika Young Africans kwenye Uwanja wa Sokoine jijini
Mbeya.
Kagera Sugar kwa upande wake Jumapili itacheza na Ruvu Shooting
kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, ilihali JKT Ruvu itakuwa mwenyeji
wa Toto Africans kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani
Pwani.
Ligi hiyo itaendelea Jumatatu kwa michezo miwili ambako Mtibwa Sugar
itaialika Mbeya City kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Morogoro wakati
Mwadui itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Mwadui
ulioko Shinyanga.
Leave a Comment