"TULITUMIA MBINU YA ITALIA KUWAMALIZA SIMBA" - KOCHA WA LYON AMEYASEMA HAYA
Kocha mkuu wa African Lyon Bernardo Tavares amesema waliamua kutumia
style ya Italia kuimaliza Simba kwenye mchezo wa jana Jumapili na
kufanikiwa kuondoka na pointi tatu mbele ya Simba ambao kabla ya mchezo
huo walikuwa hawajapoteza mechi katika michezo yao 13 tangu kuanza kwa
msimu huu.
Tavares hakuacha kuipongeza Simba akisema wanatimu nzuri na wachezaji
wazuri ndio maana waliweza kushinda mechi 11 na kutoka sare katika
mechi mbili kati ya 13 zilizopita.
“Kwanza nianze kwa kuipongeza Simba kwasababu ni timu nzuri, kabla ya
mchezo wetu walikuwa hawajapoteza mcezo hata mmoja, walishinda mechi 11
na sare mbili hakukuwa na timu iliyoifunga Simba, kwahiyo ni timu nzuri
yenye wachezaji wazuri.”
“Kipindi cha kwanza tulipata nafasi tatu za kufunga, mbili zikagonga ‘mtambaa panya’ wapinzani wetu pia walipata nafasi.”
“Kipindi cha pili walirudi wakiwa na mbinu ya kutumia nguvu na
kutushambulia lakini tuliweza kuwadhibiti kutokana na aina ya ulinzi wa
Italia tuliouweka. “
“Mbinu kwa ajili ya mchezo huu ziliwapa nafasi mabeki wangu kucheza
vizuri licha ya kuwa Simba walipata nafasi japo wengine wanaweza kusema
Simba walipata nafasi lakini hii ndio soka. Wakati mwingine unakuwa na
bahati wakati mwingine hupati bahati, sisi tulikuwa na bahati.”
Leave a Comment