TB JOSHUA ASHAMBULIWA KWA KEJELI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KWA UTABIRI WAKE FEKI
Utabiri wa mhubiri maarufu raia wa Nigeria TB Joshua, kuwa Hillary Clinton atamshinda Donald Trump umeambulia patupu
Aliandika
kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa Bi Clinton atashinda kwa kura
chache. Kwa sasa ujumbe aliouandika kwenye mtandao umefutwa na sasa
watu wanaendelea kumkejeli mhubiri huyo.
Mwanzilishi huyo wa The Synagogue Church of nations (SCOAN), alisema ameona ufunuo huo siku 10 kabla ya uchaguzi.
TB Joshua ni mmoja wa wahubiri maarufu na wenye kukumbwa na utata
barani Afrika huku wengi wa wafuasi wake wakiamini kuwa utabiri wake ni
wa ukweli.
Haya ni baadhi ya maneno ya kejeli waliyoandika wanaijeria katika mtandao wakijamii wa Twitter.
Leave a Comment