HILARY CLINTON: NIMESHINDWA, HONGERA DONALD TRUMP
CNN na NBC wameripoti kwamba mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton amempigia simu Donald Trump na kukubali kushindwa.
Trump amepanda jukwaani Manhattan, New York. Amewashukuru wafuasi wake
na kusema amepigiwa simu na Hillary Clinton "kuwapongeza".
George W Bush amesema hakupigia Clinton au Trump kura ya urais. Shangwe, nderemo na vifijo zimetanda miongoni mwa wafuasi wa Donald Trump.
Wafuasi wa wagombea wakuu wa urais nchini Marekani Hillary Clinton na
Donald Trump wamepokea matokeo yanayoendelea kutangazwa kwa hisia
tofauti mjini New York.
Matokeo ya uchaguzi mkuu wa kuamua rais wa 45 atakayemrithi Rais Barack
Obama mwakani yanaendelea kupokelewa. Wagombea wawili wakuu ni Donald
Trump wa Republican na Hillary Clinton wa Democratic.
Chama cha Republican kimeshinda viti vingi katika bunge la Seneti ya Marekani .
Siri za jamii inaendelea kufuatilia hotuba inayotolewa na Donald Trump na itaiwasilisha hivi punde ili msomaji uendelee kupata habari kamili
Leave a Comment