MUNGU MWANAMKE WA INDIA APIGA WATU RISASI NA KUJERUHI HARUSINI
Sadhvi Deva mwanamke anayejiita Mungu
Polisi nchini India wanamtafuta
Sadhvi Deva Thakur, mwanamke aliye mafichoni baabda ya kufyatua risasi
za kusherehekea kwenye harusi
Shaghaziye bwana harusi aliuawa huku watu wengine watatu wakijeruhiwa vibaya.
Kwenye
video ya tukio hilo lililotokea siku ya Jumanne katia jimbo la
Kaskazini la Haryana, Sadhvi Deva Thakur anaonekana akifyatua risasi
akitumia bunduki aina ya revolver.
Mwanamke huyo alimuomba DJ kwenye harusi hiyo aupige wimbo anaoupenda huku akiendelea kufyatua risasi ndipo shangazi wa bwana harusi alianguka chini kwa kupigwa risasi na wengine watatu wamejeruhiwa vibaya.
Polisi wamewafungulia kesi ya mauaji na wanaendelea kuwatafuta wahusika saba wa tukio hilo.
Leave a Comment