MGOMBEA URAIS MAREKANI DONALD TRUMP ATOLEWA JUKWAANI KUHOFIA KUPIGWA RISASI

Zikiwa zimekaribia siku chache uchaguzi mkuu ufanyike nchini Marekani, matukio ya kustaajabisha na kushangaza huwa hayakosekani.

 Donald Trump akiondoshwa jukwani na maafisa usalama
Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican bwana Donald Trump, ametolewa jukwaani na walinzi wake wa karibu kulinda usalama wake dhidi ya mfuasi mmoja aliyedhaniwa ana silaha.
Mtu mmoja aliropoka kuwa ana silaha na Trump angepigwa risasi muda wowote hali ambayo ilisababisha taharuki kubwa baina ya makutano hayo. Mtu huyo alifanikiwa kukamatwa lakini aliachiwa hapo baadae kwani hakukutwa na silaha kama ilivyodhaniwa.
Tukio hilo lilitokea kwenye ukumbi wa Reno mji wa Nevada ambapo Trump alikuwa anafikia kilele cha hotuba yake kabla ya kutokea tafrani hiyo.
Huku zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya uchaguzi mkuu, wagombea wote wawili wameimarisha kampeni zao katika jimbo muhimu la Florida ambalo lina umaarufu wa kuamua mshindi wa uchaguzi wa urais.
Kumekuwa na ongezeko la watu wa asili ya hispania wanaopiga kura mapema Florida na Nevada.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema huenda hatua hiyo ikamnufaisha Bi Clinton.
Trump amesema atazuru jimbo la Minnesota ambalo chama cha Republican hakijawahi kupata ushindi kwa zaidi ya miaka arobaini

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.