MESSI AFIKISHA MABAO 500 , SUAREZ AMUANDIKIA UJUMBE KWENYE MTANDAO WA TWITTER! SOMA HAPA KUUONA UJUMBE HUO


Barcelona sasa wanacho kingine cha kutunza katika record zao baada ya mshambuliaji wao machachari Lionel Messi kuweka record mpya baada ya mchezo wao wa jana dhidi ya sevilla. Muargentina huyo alifunga bao lake la 500 akiwa na klabu yake ya barcelona. Mshambuliaji huyo mwenye miaka 29 aliweka bao la kwanza katika ushindi wa mabao 2 - 1 dhidi ya sevilla.
Messi aliweka bao lake la kwanza na timu ya wakubwa ya miamba hiyo ya hispania mwaka 2005 na tangia hapo amekuwa mtu anayeisadia klabu yake kutwaa mataji makubwa barani ulaya.
Luis Suarez nae hakuwa nyuma kumpongeza rafiki yake huyo baada ya kumuandikia ujumbe kwenye twitter.


No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.