MAJARIBIO YA CHANJO YA UKIMWI KUFANYIKA AFRIKA KUSINI


Chanjo mpya dhidi ya virusi vinavyosababisha Ukimwi itaanza kufanyiwa majaribio nchini Afrika Kusini Jumatano wiki hii.
Wanasayansi wanasema huenda ikawezesha binadamu kukabiliana na virusi hivyo iwapo itafanikiwa, shirika la habari la AP linasema.
Wakati wa majaribio hayo, ambayo yamepewa jina HVTN 702, wanasayansi wanatarajiwa kuwatumia wanaume na wanawake 5,400 ambao wanashiriki ngono kutoka maeneo 15 nchini Afrika Kusini.
Washiriki hao watakuwa wa umri wa kati ya miaka 18 na 35.
Majaribio hayo yatakuwa makubwa zaidi na ya kina zaidi ya chanjo ya Ukimwi kuwahi kufanyika nchini Afrika Kusini.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.