LIGI KUU BARA : SIMBA NA AZAM WANA KIBARUA KIZITO MBELE YAO LEO HII
Ligi kuu ya Tanzania bara itaendelea tena leo kwa michezo miwili kupigwa katika miji ya Shinyanga na Mbeya.
Vinara
wa ligi hiyo wekundu wa Msimbazi Simba, watakua ugenini mkoani Mbeya,
kusaka alama tatu muhimu kwa kucheza na Tanzania Prisons,mchezo
utakaopigwa katika dimba la Sokoine.
Azam Fc, nao watakua katika uwanja wa ugenini huko mkoani Shinyanga kwa kucheza na Mwadui FC.
Ligi
hiyo itaendelea tena kesho Alhamisi kwa mchezo mmoja ambapo
mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga, wa watawakaribisha Ruvu Shooting,
mchezo utakaopigwa katika dimba la Uhuru jijiji Dar es Salaam.
Leave a Comment