KOCHA WA MAREKANI JURGEN KLINSMANN AFUKUZWA KAZI
Mchezaji wa zamani na meneja wa Ujerumani Jurgen Klinsmann ametimuliwa katika nafasi ya ukocha wa timu ya taifa ya Marekani.
Klinsmann mwenye miaka 52 aliyeshinda kombe la dunia akiwa mchezaji mwaka 1990 alianza kukinoa kikosi cha Marekani mwaka 2011.
''Tunaendelea
kuwa imara, tuna wachezaji wa kiwango cha juu wa kutusaidia kufuzu
kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi,'' amesema Rais wa shirikisho la
soka nchini Marekani Sunil Gulati.
Klinsmann aliifikisha Marekani hatua ya 16 katika kombe la dunia 2014 nchini Brazil.
Sambamba
na hilo walipoteza kwa magoli 2-1 wakiwa nyumbani dhidi ya Mexico na
baadae kufungwa 4-0 na Costa Rica katika hatua ya kufuzu kombe la dunia.
Marekani inabakia mkiani mwa timu sita ikiwa haina alama yoyote.
Klinsmann
mshambuliaji wa zamani wa Tottenham alihusishwa kuinoa timu ya taifa ya
England baada ya Sam Allardyce kubwaga manyanga mwezi Septemba.
Leave a Comment