DONALD TRUMP AZITOLEA UFAFANUZI SERA ZAKE NA VIPAUMBELE VYAKE
Rais mpya wa Marekani Donald Trump
Baada ya mkutano na msemaji wa
Republican Paulo Ryan, rais mteule wa Marekani Bwana Donald Trump
ameeleza vipaumbele vya sera zake.
Mteule huyo amesema atapunguza
kodi na kufanya mageuzi ya sekta ya huduma za afya kwa kuachana na
mfumo uliowekwa na Barack Obama.
Pia amesema atabadili haraka
sheria juu ya uhamiaji , Hizo ni miongoni mwa hatua tatu muhimu
alizoahidi kwenye kampeni zake za Urais.
Alisema yeye atafanya mambo ya kuvutia kwa ajili ya watu wa Marekani.
Lakini baadhi ya ahadi alizotoa kwenye kampeni zimeondolewa kwenye
tovuti yake ikiwemo tishio la kupiga marufuku Waislamu kuingia
Marekani, kuachana na makubaliano ya Paris katika kupambana na
mabadiliko ya hali ya hewa.
Kampeni za Trump zisingeweza kusema kuhusu mabadiliko hayo ya tovuti
Leave a Comment