ARSENAL VS TOTTENHAM: ARSENAL NI MBABE WA TOTTENHAM, TIZAMA REKODI HIZI

Leo katika viwanja mbali mbali nchini uingereza, kabumbu litakuwa likipigwa baina ya timu mbali mbali katika kutetea points kwenye msimamo wa ligi. Moja ya mchezo utakaovutia watizamaji wengi ni mchezo kati ya Arsenal na Tottenham ambao utapigwa kwenye uwanja wa Emirates Stadium.
Arsenal amefanikiwa kuibuka mbabe mara nyingi zaidi ya Tottenham katika mechi zao zote walizokutana. Kwenye mechi 191 ambazo timu hizo zimekutana, Arsenal wameshinda mara 80, Spurs mara 61 na 50 zimemalizika kwa sare. 


Tangu awe meneaja wa Arsenal, Arsene Wenger amecheza michezo 48 ya Premier League dhidi ya Spurs na kushinda mara 22- sawa na uwiano wa asilimia 46, ametoka sare mara 19, kwa maana kwamba ameweza kujinyakulia pointi kwa asilimia 85 ya mechi dhidi ya mahasimu wao hao.
Arsene Wenger ameyafurahia sana maisha ya kuifundisha timu ya Arsenal kwa miaka 20 sasa. 

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.