ZITAMBUE RECORDS MPYA MUHIMU ZILIZOWEKWA KATIKA HISTORIA YA MPIRA BAADA YA MECHI YA BARCELONA NA MANCHESTER CITY
Mpira wa miguu ni moja ya mchezo unaoteka sana hisia za watu hususan pale matukio ya kihistoria yanapofanyika uwanjani. Hapo jana October 19, katika moja ya michezo iliyovutia watizamaji wengi ni mechi kati ya Barcelona na Manchester City. Wenyeji wa mechi hiyo Barcelona walifanikiwa kuondoka na ushindi mnono wa mabao 4 kwa sifuri ikiwa ni ukaribisho mbaya wa Pep Guardiola tangu alipoachana na klabu hiyo.
Star wa mchezo huo Lionel Messi alionesha makali yake kwa kuingia wavuni mara tatu kutokana na kukosekana kwa umakini katika ngome ya Manchester City.
Lionel Messi katika moja ya magoli aliyofunga akiwakabili Manchester City
Na hizi ni rekodi muhimu unazohitaji kuzijua baada ya mchezo wa Barcelona na Manchester City:
- Lionel Messi amefunga mabao 15 katika mechi zake 13 alizocheza na timu za Uingereza
- Manchester City imepokea kipigo kikubwa cha magoli kwa mara ya kwanza katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya kwa kuruhusu magoli manne (4).
- Goli la kwanza la Messi lilikuwa la 100 akiwa kwenye combination ya Neymar na Suarez.
- Messi sasa ni mchezaji anayeongoza kwa kufunga mabao mengi zaidi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya katika uwanja wa nyumbani, mabao 50.
- Barcelona amepoteza penati 11 kati ya 27 katika michuano yote tangu kuanza kwa msimu 2015/2016.
Leave a Comment