UCHAGUZI WA REFA ATAKAYECHEZESHA MPAMBANO WA LIVERPOOL NA MANCHESTER UNITED WAZUA GUMZO
Jumatatu ya juma lijalo patakuwa na mtanange mkubwa kwenye ligi ya uingereza kati ya mahasimu wakubwa Liverpool na Manchester United. Kuelekea kwenye mpambano huo, refa aliyechaguliwa kuwa mwamuzi wa kati wa mchezo huo Anthony Tylor, amepingwa vikali na wadau mbalimbali wa mpira pamoja na mashabiki wa liverpool.
Aliyekuwa chief wa marefa nchini Uingereza Keith Hacket, amedai kwamba makazi ya Anthony Tylor yanaweza yakawa ni sababu ya utata kutokea kwani anaishi maili sita tu (6 miles) kufika Old trafford. "Hakuna mwenye shaka na uwezo wake na uaminifu wake wa kazi, lakini itakuwaje likitokea tatizo lolote? Ukaribu wake na eneo la Old Trafford inaweza ikawa sababu" anasema Keith Hacket.
Nao mashabiki wa liverpool hawakuwa nyuma kutupa lawama mitandaoni kwa kile kinachoonekana kama si haki kwao, hizi ni baadhi ya tweets walizoweka katika mtandao wa kijamii wa twitter.
Aidha bodi inayohusika na uchaguzi wa marefa (PGMOL), wamekanusha madai kwamba makazi ya refa sio sababu wala haidhuru uchaguzi wa refa kuchezesha mechi yoyote.
Leave a Comment