SIMBA YACHOSHWA NA UBABAISHWAJI NA YANGA KATIKA SAKATA LA KESSY


Hassan Ramadhani Kessy
Endapo Simba na Yanga watashindwa kufikia makubaliano watarudi kwenye kamati na kutolewa maamuzi kulingana na kanuni zilizopo
Klabu ya Simba imeliomba Shirikisho la soka Tanzania TFF, kulirudisha swala la mchezaji Hassan Ramadhani ‘Kessy’ kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ili liweze kupatikana muafaka.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hans Poppe ameiambia Goal,wamechoshwa na namna ya ubabaishwaji wa watani zao Yanga ambao kila kukicha wamekuwa na sababu mpya ambazo zinawafanya kushindwa kulimaliza jambo hilo.
“Kama Yanga wangekuwa wanataka suala hili liishe mapema wagetumia kipindi hiki kukutana nasi lakini licha ya kamati kututaka tumalizane wenye wamekaa kimya na hatujui wanampango gani ndiyo maana tunaona turudi huko kwenye Kamati tunaamini haki itapatikana,”amesema Hans Poppe.
Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ilizitak timu hizo kukutana na kulimaliza swala hilo lakini endapo watashindwa kufikia makubaliano watarudi kwenye kamati na kutolewa maamuzi kulingana na kanuni zilizopo.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.