MTANGAZAJI WA CLOUDS FM PJ ABURUZWA MAHAKAMANI NA EFM RADIO

PJ aliondoka EFM mwanzoni mwa mwezi Oktoba na kurejea Clouds FM alikokuwa akifanya kazi kabla ya kuondoka pamoja na mtangazaji mwenzake Gerald Hando.
EFM imefungua mashtaka katika Mahakama ya Kazi jijini Dar es Salaam kwa madai ya kukiuka mkataba wa kazi na kituo hicho.
Kufuatia mashtaka hayo, EFM inadai fidia ya pesa kiasi cha Tsh. Milioni 200 kutoka kwa mtangazaji huyo.
Inadai PJ alikatisha mkataba kiholela na
kurudi tena Clouds FM bila kufuata makubaliano pamoja na sheria
alizokubaliana nazo katika mkataba wake pale alipojiunga nacho.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa November 23, 2016 katika Mahakama ya Kazi ya jijini Dar es Salaam.

source:
Leave a Comment