MTANGAZAJI ALIYEMHOJI DONALD TRUMP ASIMAMISHWA KAZI SHIRIKA LA NBC
Mtangazaji wa shirika la utangazaji NBC, Bwana Billy Bush amesimamishwa kazi na shirika hilo kufuatia kufichua mkanda wa mahojiano baina yake na mgombea wa sasa wa urais kupitia chama cha Republican, Donald Trump miaka kumi iliyopita (2005). Mkanda huo ulimuonesha Donald Trump akiwadhalilisha wanawake kwa matamshi yake.
Bwana Billy Bush
Baada ya kuvujishwa kwa mkanda huo viongozi wengi wa juu wa chama cha Republican wamekuwa wakimtenga Donald Trump. Kwenye video hiyo bwana Billy Bush ameonekana akicheka kutokana na matamshi aliyokuwa akiyatoa Bwana Donald Trump ya kuwadhalilisha wanawake.
Mke wake Trump, Bi Melanie amemshutumu mtangazaji huyo akidai kwamba alimchochea mumewe kutoa matamshi hayo na mumewe ni mtu anayeheshimu sana wanawake.
Billy Bush (45) ni mpwa wa aliyekuwa rais wa marekani George Bush, alikuwa anatangaza kipindi cha "TODAY" katika shirika la utangazaji la NBC, na mkanda huo ulivujishwa na majuzi na gazeti la Washington Post.
Aidha , Billy Bush ameomba radhi kwa tukio hilo na kudhihirisha amesikitishwa na kujutia kosa hilo.
Leave a Comment