VAN DER PLUIJM: MWASHIUYA ATAKUWA KAZINI OKTOBA MOSI DHIDI YA SIMBA

Mwashiuya aliumia goti kwenye mchezo wa Kombe la
Shirikisho Afrika dhidi ya Madeama, lakini daktari wa Yanga amesema
mchezaji huyo sasa ameimarika
Pluijm , Mwashiuya yupo Pemba walipoweka kambi kujiandaa na mchezo wa Simba na amemwandilia program maalumu kuhakikisha anakuwepo kwenye kikosi cha wachezaji 18 watakao husika kwenye mchezo huo wa Oktoba 1.
“Tunaye hapa Pemba na kitu kizuri nikwamba ameonyesha mabadiliko ya haraka pamoja na kukaa nje kwa muda mrefu imani yangu anaweza kupata japo dakika 10 kwenye mchezo wa Jumamosi," amesema Pluijm.
Mwashiuya aliumia goti kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Madeama ya Ghana uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam, na Pluijm anataka kumtumia kwasababu ndiyo mtengenezaji wa bao la pili lililofungwa na Amissi Tambwe kwenye mchezo uliopita wa Yanga na Simba uliopigwa Febuari 20, 2016.
Leave a Comment