UTARATIBU WA KUSAJILI NDOA IKIWA UMEISHI NA MWANAMKE KWA MUDA BILA NDOA
Utaratibu wa Kusajili Ndoa.
Ndoa yeyote iliyofungwa lazima isajiliwe na wanandoa kupewa cheti cha ndoa mara tu
baada ya kufunga ndoa.
Iwapo ndoa ilifungwa kimila na haikusajiliwa, wanandoa wanaweza kufanya usajili wa
ndoa hiyo kwa kuwasilisha maombi kwa msajili wa wilaya, kadhi au afisa msajili yeyote:
• Mwombaji ataandaa taarifa ya uthibitisho wa kuwepo kwa ndoa hiyo.
• Atawasilisha maombi na uthibitisho huo kwa msajili wa wilaya na afisa msajili.
• Cheti cha ndoa kitatolewa baada ya afisa msajili kuridhika na uthibitisho uliotolewa.
Jambo la kuzingatia
Uthibitisho wa kuwepo kwa ndoa unaweza kutolewa kwa barua ya utambulisho
inayothibitisha kufungwa kwa ndoa husika iliyotolewa na taasis au chombo cha kidini
au ushahidi wa majina ya mfungishaji,
Ni muhimu na ni utaratibu wa kisheria kusajili ndoa.
Ni muhimu kuwa na cheti za usajili wa ndoa kwani ni utambulisho na uthibitisho wa
kuwepo ndoa halali.
Leave a Comment