UNAIJUA SIRI YA KOCHA WA CHELSEA KABLA NA BAADA YA MECHI? INGIA SIRINI UZIJUE .......
Hapo jana majira ya saa nne usiku kwa Africa Mashariki, kulikuwa na mtanange mzito baina ya timu mbili za Liverpool na Chelsea. Chelsea ilijikuta ikiangukia pua katika mchezo huo kwa kupoteza kwa idadi ya magoli 2 - 1, magoli ya liverpool yamewekwa kimyani na Dejan lovren pamoja na Jordan Henderson kwa shuti maridadi kabla ya mda wa mapumziko, bao la chelsea lilifungwa na mshambuliaji wao hodari mtukutu Diego Costa.
Antonio Conte
Lakini wajua kocha wa Chelsea muitaliano Antonio Conte alitoboa siri gani kuhusu yeye anapokuwa anakabiliwa na mechi mbele yake? Namnukuu hapa ,
" Kabla ya mechi, mara nyingi huwa silali sana. Ninalala kwa saa 2,3 au 4 nikiamka huwa ninaanza kufikiri kuhusu mechi.
Baada ya mechi, nikishinda nalala, lakini nisiposhinda huwa ni vigumu kulala. Katikati ya usiku huwa ninafikiri, ni kwa nini tumepoteza?"
Haya maneno aliwahi kuyaongea Antonio Conte alipotua Chelsea. Baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza akiwa kama kocha wa Chelsea hapo jana, unauonaje usingizi wa Conte usiku wa kuamkia leo?
Kwa siri kama hizi na siri nyingine nyingi katika ulimwengu wa michezo, siasa, kilimo , biashara , elimu , burudani na mengine mengi, usisahau kusubscribe katika blogu yetu, ku-like page zetu za Facebook na Instagram zinazokwenda kwa jina la "Siri za Jamii"
Leave a Comment