SIRI ZA JAMII: UTARATIBU WA KUFUNGUA MIRATHI IKIWA MAREHEMU AMEACHA WOSIA AU AJAACHA WOSIA

Posted by
Jackson Msuya
14 sept, 2016
Utaratibu wa Kufungua Mirathi

IWAPO MAREHEMU AMEACHA WOSIA:
1. Lazima kifo kiandikishwe katika ofisi ya vizazi na vifo katika wilaya ambayo kifo
kimetokea. Muda wa kisheria wa kuandikisha ni siku 30 tangu kifo kilipotokea.


2. Msimamizi aliyependekezwa na marehemu kwenye wosia ndiye mwenye mamlaka ya
kufungua shauri la mirathi katika mahakama husika. Utaratibu wa kisheria unaelekeza
kuwa mirathi zote za kimila au kiislam zitafunguliwa katika Mahakama ya Mwanzo
wakati mirathi zitakazofuata taratibu za sheria ya serikali itafunguliwa Mahakama ya
Wilaya au Mahakama Kuu ya Tanzania.


3. Iwapo wosia haukumtaja msimamizi wa mirathi basi mkutano wa ukoo ukae na
kupendekeza mtu kuomba usimamizi huo.


4. Baada ya mahakama kupokea maombi ya usimamizi huo, itatoa utaratibu wa
muombaji kugharamia tangazo la mirathi katika gazeti. Tangazo hilo litatoa muda wa
siku 90 kuruhusu poingamizi toka kwa mtu yeyote anayepinga muombaji kupewa
usimamizi wa mirathi.


5. Mahakama itatoa ruhusa kwa msimamizi wa mirathi aliyeteuliwa kugawa mali kwa
kufuata wosia.


IWAPO MAREHEMU HAKUACHA WOSIA:

1. Lazima kifo kiandikishwe katika ofisi ya vizazi na vifo katika wilaya ambayo kifo
kimetokea. Muda wa kisheria wa kuandikisha ni siku 30 tangu kifo kilipotokea.


2. Mkutano wa ukoo ukae na kupendekeza jina au majina ya msimamizi wa mirathi.


3. Baada ya mahakama kupokea maombi ya usimamizi huo, itatoa utaratibu wa
muombaji kugharamia tangazo la mirathi katika gazeti. Tangazo hilo litatoa muda
wa siku 90 kuruhusu poingamizi toka kwa mtu yeyote anayepinga muombaji
kupewa usimamizi wa mirathi.


4. Msimamizi atawajibika kugawa mali ya marehemu kwa warithi waliokubalika katika
mahakama, na kwa kufuata sheria.

NAKALA AU TAARIFA MUHIMU KATIKA SHAURI LA MIRATHI:


i. Nakala ya muhtasari wa kumbukumbu wa kikao cha ukoo
ii. Nakala ya wosia, iwapo marehemu aliacha wosia
iii. Majina ya warithi halali wa mali za marehemu
iv. Cheti cha kifo
v. Cheti cha ndoa, iwapo marehemu aliacha mke/mume
vi. Vyeti vya kuzaliwa vya watoto
vii. Taarifa muhimu za marehemu: majina, tarehe ya kufariki, jina la mwombaji, orodha
ya mali alizoacha marehemu
viii. Nakala au taarifa zozote zitakazo hitajika mahakamani

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.