SIRI ZA JAMII: IJUE NDOA BATILIFU KATIKA MAISHA YETU YA KISWAHILI
Katika maisha yetu ya kitanzania unaweza kujikuta unaishi na mwanamke au mwanaume kwa ndoa halali lakini bila kujua kuwa ndoa yenu ni batilifu kwamba ni ndoa halali lakini kutokana na mambo kadhaa ambayo nitakuhamisha imeifanya kuwa batilifu kisheria.ikiwa umejikuta katika ndoa ya namna hii kama ukihisi auna furaha na ujui nini cha kufanya jua kabisa una haki zako kisheria na unaweza kupatiwa haki katika swala hili la ndoa batilifu.
NDOA BATILIFU
Kwa mujibu wa kifungu cha 39 ndoa batilifu ni ndoa halali kisheri lakini kwa sababu fulani fulani mara tu baada ya kufunga ndoa inaonekana wafunga ndoa hao hawawezi kuendelea kwenye ndoa hiyo. Mambo yafuatayo yanaweza kuifanya ndoa kuwa batilifu:

- 1: Kutoweza kufanya tendo la ndoa.
- 2: Mmoja wa wanandoa kudhihirika kuwa na kichaa au kifafa.
- 3: Mmoja wa wanandoa kudhihirika kuwa alikuwa ana magonjwa ya zinaa.
- 4: Mke kudhihirika kuwa alikuwa na mimba ya mwanaume mwingine.
- 5: Mwanandoa mmoja kukataa kwa makusudi kufanya tendo la ndoa tangu ndoa kufungwa.
- Ndoa batilifu ni ndoa halali na itaendelea kuwa hivyo hadi hapo mahakama itakapoitengua.
Leave a Comment