SHERIA YA HAKI MILIKI NA SHIRIKISHI NCHINI TANZANIA ITAMBUE HAPA
KATIKA mambo yanayowasumbua watu
wengi duniani (Tanzania ikiwemo) ni suala la hakimiliki na hakishiriki kwa
wasanii na wabunifu wa sanaa.Hapa nchini, baada ya sheria ya hakimiliki ya
mwaka 1966 kuthibitika kwamba ina mapungufu mengi, ndipo mwaka 1999 Bunge la
Jamhuri ya Muungano lilipotunga sheria mpya ya hakimiliki na hakishiriki, namba
7 ya mwaka 1999, yenye sura ya 218 ya sheria za Tanzania (kama
zilivyorekebishwa mwaka 2002).
Kwa mujibu wa utangulizi wa sheria
hii, imeletwa kutengeneza na kutoa manufaa zaidi na ulinzi zaidi wa kazi za
wasanii wa kazi zinazolindwa na haki miliki na hakishiriki na zingine zote
zinazoendana na hizo.Chini ya kifungu cha 2(c) cha sheria hii, ambacho kimsingi
kinazungumzia madhumuni ya kutungwa kwa sheria hii ya muhimu kwa maendeleo ya
wasanii na watunzi na wabunifu wote katika nyanja za nyimbo, maigizo na tasnia
nyingine zinazoendana na hizo.Sheria hii ina madhumuni ya kuinua kazi za fasihi
na za kisanii pamoja na nyinginezo zinazofanana na hizo.
Kwa mujibu wa sheria hii, kuna
makundi makubwa mawili ya haki za wasanii zinazolindwa na sheria hii, ambazo ni
haki ya kiuchumi na haki za kitamaduni ambazo mtunzi wa kazi zinazolindwa na
sheria hii ana haki nazo.
Haki hizi zina msingi katika mkataba
wa kimataifa wa Benne wa mwaka 1883 ulioridhiwa na Tanzania Julai 25, 1994; na
hivyo kwa mujibu wa kanuni za kisheria za kimataifa, Tanzania ina wajibu wa
kutimiza yaliyomo katika mkataba huu iliyouridhia.Kwa mujibu wa sheria hii,
chini ya kifungu cha 3(i) cha sheria hii, kazi zinazolindwa na sheria hii ni
zile ambazo zimetengenezwa na mtunzi wa Kitanzania au zile ambazo mtunzi wake
si Mtanzania lakini ana makazi yake ya kudumu hapa nchini au kazi hiyo
iliyotengenezwa kwa mara ya kwanza hapa Tanzania, au kazi ambazo ni za kusikika
na kuona (audio-visual) ambazo mtayarishaji wake ni Mtanzania au makao makuu
yake yakutengeneza kazi hizo zipo nchini.
Na kwa mujibu wa kifungu cha 3(3)
cha Sheria hii wasanii wanaomiliki kazi za kisanii na wana hakishiriki pia
watapewa ulinzi na sheria hii.Katika kifungu cha 4, msanii ametafsiriwa kama
mwigizaji, mwimbaji, mwanamuziki, mchezaji (dancer) au mtu anayeigiza, kuchonga
au kufanya maonesho jukwaani.
Hata hivyo, sheria hii kama sheria
nyingine nyingi za hakimiliki, imetoa sharti kwa kazi za kisanii kulindwa na
sheria hii na kigezo hiki ni kwamba kazi hiyo iwe katika hali ya kushikika, na
kwa maana nyingine ni kwamba wazo/mawazo hayatalindwa na sheria hii hata
kidogo.
Kwa mfano, kama A na B walio katika
sehemu tofauti lakini wana wazo linalofanana la kutengeneza wimbo unaohusu
foleni za magari, na A akawa wa kwanza kuingiza wimbo huo katika hali ya
kushikika (katika minajili hii akawa ameurekodi studio), basi B hawezi kuja
kumshitaki A kwa kuiba wimbo wake kwani yeye alikuwa na wazo tu na wakati
mwenzake aliliweka katika hali ya kushikika.
Hii ina maana kwamba, kazi ya
kisanii haitalindwa na sheria hii kwa njia ya kusajili kazi hiyo, bali kwa njia
ya kuiweka kazi yenyewe kuwekwa katika hali ya kushikika.
Kifungu cha 5 cha sheria hii
kinaorodhesha baadhi ya kazi zinazolindwa ikiwa ni pamoja na kazi za sinema na
michezo ya sinema, mihadhara, vitabu, majarida, kazi za muziki,upigaji wa picha
za kawaida, ramani na picha za kuchonga na kadhalika.
Kifungu hiki kinaendana na maamuzi
ya Mahakama ya Uingereza katika shauri la University of London Press Ltd dhidi
ya University Tutorial Press, (1916) 2 Ch.601 ambapo nayo ilitafsiri nini ni
kazi ya kisanii kumaanisha yaliyomo katika kifungu cha 5 cha sheria ya
hakimiliki na hakishiriki ya Tanzania.Kwa upande mwingine, sheria hii imetaja
baadhi ya kazi ambazo haziwezi kulindwa na sheria hii ikiwa ni pamoja na habari
zinazochapishwa/tangazwa katika vyombo vya habari, sheria na maamuzi ya vyombo
vya kutoa maamuzi kama mahakama na mabaraza, na pia wazo la aina yeyote ambalo
halijawekwa katika hali ya kushikika na kudumu, kama ambavyo wenzetu wa
Uingereza walivyolipatia ufumbuzi katiak shauri la Springfield dhidi ya Temp,
(1903) 19 TLR 650, ambapo mahakama iliamua kwamba wazo la aina yeyote haliko
katika ulinzi wa sheria ya haki miliki wala hakishiriki.
Haki ya kiuchumi kama tulivyoona
hapo awali, katika sheria ya Tanzania, inapatikana chini ya kifungu cha 9, na
haki hii ni ile haki ambayo mtunzi wa kazi inayolindwa na sheria hii amepewa
kuwa na haki zote juu ya kazi yake, katika masuala yote yanayohusiana na
kutafsiri kazi yake, kuikodisha, kuionesha katika umma, kuionesha katika vyombo
vya habari, kuisambaza, kuitumia hadharani na kadhalika.
Haki hizi upatikana kwa kufata misingi ya sheria za nchi najua wewe anko wangu unaitaji kuwa msanii na kufanya kazi za sanaa na ndio maana anko wako nikaona nikusogezee kitu cha kuongeza ufahamu kama msanii na kukuza sanaa yako sio tu kwenye kipaji bali na kimaarifa pia.
Leave a Comment