MUAMUZI MARTIN SAANYA KUAMUA MECHI YA SIMBA NA YANGA


Martin Saany - Mwamuzi Tanzania


Mwamuzi huyo ana beji ya FIFA na itakuwa mara yake ya pili kuchezesha mechi kubwa ya Yanga dhidi ya Simba, mara ya kwanza Yanga ilishinda mbili bila
Wakati zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya miamba ya soka Yanga na Simba kupambana kwenye mchezo wa ligi ya Vodacom Shirikisho la soka Tanzania TFF, limemteua mwamuzi, Martin Saanya kutoka Morogoro kuchezesha pambano hilo kubwa Jumamosi.
Mwenyekiti wa Bodi ya ligi Boniface Wambura, amesema, wamemteua Saanya kuchezesha pambano hilo kwakua ana beji ya Shirikisho la soka duniani FIFA, na ana uzoefu mkubwa katika kuchezesha mechi kubwa kama hiyo.
“Tumemteua Saanya kwa sababu tunataka kumaliza utata mara nyingi timu hizi zimekuwa na malalamiko timu moja inapopoteza mchezo dhidi ya mwenzake na lawama kubwa hutupiwa mwamuzi sasa Saanya ana beji ya FIFA, tunaamini atachezesha vizuri na kila upande utaridhika,” amesema Wambura.
Hiyo itakuwa ni mara ya pili kwa Saanya kuchezesha mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga, mara ya kwanza alizichezesha timu hizo msimu wa 2013/14 na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.







S

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.