MICHEZO: UNAZIFAHAMU SIRI HIZI ZA MANCHESTER UNITED INAPOKUTANA NA WATFORD? HII NI SPECIAL KWENU KABLA YA KUTAZAMA MECHI YA LEO .....

Leo hapo baadae mchana Manchester United itashuka dimbani nyumbani kwa Watford katika mchezo wa ligi kuu Uingereza. Ikumbukwe pia Mashetani hawa wekundu wamepoteza mechi mbili mfululizo kufuatia kufungwa na mahasimu wao Manchester City, na Fayenoord ya uholanzi katika michuano ya Europa. Wakati huo wapinzani wao wa leo Watford wamejiweka nafasi nzuri baada ya kuwagalagaza Westham united kwa mabao 4 - 2.  Kuelekea mchezo wa leo kocha wa Manchester United Jose Mourinho katika mahojiano na BBC Sports, amedai ana kikosi kizuri chenye ari kubwa ya ushindi, lakini je unaijua siri ya Mourinho na Watford? Tuendelee hapa:-

 Jose Mourinho
 
Mourinho ameshinda mechi zake zote tatu za nyuma alizocheza na Watford kwa idadi ya mabao nane, hivyo kumweka katika nafasi nzuri ya kushinda mchezo wa leo na kutuliza hasira za mashabiki.
Pia exclusive nyingine hot hot mtu wangu wa sirini ni kwamba endapo mshambuliaji Wayne Rooney ataweza kufunga katika mchezo wa leo, itamfanya kuwa mshambuliaji anayeongoza kwa kufunga magoli mengi ya ugenini katika ligi kuu ya uingereza, kwa sasa idadi ya magoli yake ya ugenini yako sawa na gwiji Alan shearer kwa idadi ya magoli 87.

 Mshambuliaji Wayne Rooney

Usisahau kusubscribe katika blogu yetu, kulike, comment na kushare katika page zetu za Facebook na Instagram zinazokwenda kwa jina la "Siri za jamii" ili kuendelea kupata siri zaidi katika nyanda zote za michezo, burudani, siasa, na mambo yanayoizunguka jamii yetu.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.