MANENO YA MAKOCHA NA WACHEZAJI KUELEKEA MCHEZO WA KESHO SIMBA V YANGA


Hans van der Pluijm
Presha ya homa ya pambano la Yanga na Simba imezidi kupanda kila upande ukijitapa kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa J'mosi


YANGA: NUKUU ZA HANS VAN DER PLUIJM NA NADIR "CANNAVARO" HAROUB

Kocha Hans Pluijm wa Yanga amesema mchezo huo hauwapi presha kwenye kambi yao kwani Simba ni timu ya kawaida kama ilivyo timu nyingine na ndiyo maana wamekuwa wakifanya mazoezi mepesi ili kujiandaa kuchukua pointi zao tatu kama ilivyokuwa msimu uliopita.
Pluijm amesema, pamoja na kusajili wachezaji wengi wapya lakini hajaona mabadiliko ya wapinzani wao licha ya kushinda mechi tano za ligi ya Vodacom na hilo watalidhihirisha Jumamosi watakapokutana uwanja wa taifa.
“Nikweli tumepoteza mchezo mmoja dhidi ya Stand lakini hainamaanishi kwamba na Simba watatufunga inawezakana Stand waka bora kuliko Simba, ndiyo maana kama kocha nimekuwa nikitoa maelekezo ya kawaida kwa wachezaji wangu kwasababu naamini tutashinda,”amesema Pluijm
Mdachi huyo amesema msimu uliopita alivuna pointi sita na mabao manne kutoka kwa Simba msimu huu anataka kutengeneza rekodi nyingine kwa kuchukua pointi sita na mabao 10 katika mechi zote mbili.


Kwaupande wake nahodha wa Yanga Nadiri Haroub ‘Cannavaro’ amewataka mashabiki wa timu hiyo kuondoa hofu na kufika kwa wingi uwanjani Jumamosi ili kushuhudia wakiifunga Simba kipigo cha aibu.
Cannavaro ameiambia Goal, anajua timu wanayokutana nayo imejidhatiti lakini mapungufu waliyokuwa nayo hayawezi kuwapa ushindi mbele ya kikosi chao bora ambacho kinarekodi nzuri dhidi ya timu inayokutana nayo Simba
“Nawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi ni mchezo mzuri na wenye ushindani lakini baada ya dakika 90 Yanga ndiyo atakuwa mshindi kama ilivyokuwa msimu uliopita na hilo linatokana na ubora wa kikosi chake licha ya kwamba tumeoteza mchezo wao hawajapoteza,”amesema Cannavaro.



SIMBA: NUKUU ZA JOSEPH OMOG NA JONAS MKUDE

Naye kocha wa Simba Joseph Omog, amesema nimchezo mgumu kwasababu unazikutanisha timu zenye upinzani mkubwa lakini anaamini timu yake itapata ushindi kutokana na kasi waliyoanza nayo msimu huu.

Omog raia wa Cameroon amesema, ushindi walioupata dhidi ya Azam umempa matumaini ya kubaini kuwa timu yake inaweza kupata matokeo mbele ya timu kubwa kama Yanga na hilo ndilo linampa matumaini ya kushinda mchezo huo.
“Ninazitaka pointi tatu za Yanga najua haitakuwa kazi rahisi kutokana na uimara wa wapinzani wetu lakini nimekiandaa kikosi changu kwa ajili ya kupambana kwa dakika zote na kupata matokeo zaidi tutaona baada ya dakika 90,” amesema Omog.

Kwaupande wake nahodha wa Simba Jonas Mkude amesema wamejipanga kufuta uteja kwa kuifunga Yanga Jumamosi kutokana na maandalizi waliyofanya na kasi waliyokuwa nayo hivi sasa.
Mkude amesema,kwa kikosi walichokuwa nacho msimu huu haoni sababu ya kushindwa kuifunga Yanga kwasababu wao ndiyo timu bora kwa sasa tofauti na ilivyokuwa kwa wapinzani wao na ndiyo maana wanaongoza ligi huku wakiwa hawajapoteza hata mchezo mmoja.
“Simba ndiyo bingwa msimu huu na Jumamosi ndiyo tutathibitisha haya ninachoweza kusema nimchezo wenye ushindani lakini uhakika wa ushindi ni mkubwa kutokana na ubora tuliokuwa nao sisi Simba msimu huu,”amesema Mkude
Huo nimchezo wa kisasi kwasababu Simba iliyopoteza mechi zote mbili msimu uliopita haitakubali tena matokeo kama yale na ndiyo maana imefanya usajili mzuri wa kusajili wachezaji wapya 11, ili kurudi kwenye ushindani kama ilivyokuwa kwa wapinzani wao Yanga
source:goal.com

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.