MADEREVA WA KITANZANIA WA MALORI 12 WATEKWA NYARA CONGO NA MALORI YAO KUCHOMWA MOTO
Hii ndio hali halisi ilivyokuwa |
Watekaji
hao walitoa saa 24 kuanzia kuanzia jioni ya September 14 wakitaka
walipwe fedha kiasi cha dola za Kimarekani 4,000 kwa kila dereva ili
waweze kuwaachia pia walitishia kuwaua mateka hao endapo hawatalipwa
kiasi hicho cha fedha walichokitaka mpaka kufikia jioni ya leo.
Taarifa za mwanzo zimedai kuwa madereva wawili kutoka Tanzania walifanikiwa
kutoroka na ndio waliotoa taarifa za kuhusu tukio hilo. Serikali kupitia
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema
imeshachukua hatua za awali za kuwasiliana na Serikali ya DRC ili
kuhakikisha kuwa madereva hao wanaachiwa haraka iwezekanavyo wakiwa
salama kabisa.
Leave a Comment