HII NDIO HESHIMA ALIOPEWA NAHODHA WA AZAM FC JOHN BOCCO MWEZI HUU AGOSTI

John Bocco, nahodha wa Azam FC amekuwa na mchango
mkubwa kwa timu yake na ndiye mwamuzi mkubwa wa matokeo waliyopata msimu
huu Ligi Kuu
Bocco ambaye pia ni nahodha wa Azam FC aliwashinda wachezaji Mzamiru Yasin wa Simba na Said Kipao wa JKT Ruvu. Katika mechi mbili ilizocheza katika mwezi huo, Bocco aliifungia timu yake mabao matatu likiwemo la kusawazisha dhidi ya African Lyon.
Alifunga mabao mengine mawili kwenye ushindi wa mabao 3-0 wa timu yake dhidi ya Majimaji. Katika mechi hizo mbili, Azam FC ilifanikiwa kupata pointi nne kati ya sita.
Mwezi huo ulikuwa na raundi mbili tu za Ligi hiyo iliyoanza kutimua vumbi Agosti 20 mwaka huu. Kwa kushinda tuzo hiyo, Bocco atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.
Leave a Comment